Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MAANDALIZI YA UTAMADUNI KARAGWE YAZIDI KUNOGA LEO WIKI YA MAONESHO YAFUNGULIWA RASMI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Ndugu wana Karagwe na watanzania kwa ujumla, karibuni kwenye kilele cha siku ya utamaduni tarehe 21 May 2016 ambapo utamadumi wa  mnya...

Ndugu wana Karagwe na watanzania kwa ujumla, karibuni kwenye kilele cha siku ya utamaduni tarehe 21 May 2016 ambapo utamadumi wa  mnyambo utaoneshwa katika uwanja wa shule ya msingi Nyakahanga. Miongoni mwa mambo yatakayokuwepo zaidi ya ngoma za asili toka vikundi mbali mbali toka pande zote za Karagwe na Kyerwa, kutakuwa na maonesho ya malikale zinazoonyesha mchakato wa maendeleo ya Karagwe kwa kipindi kisichopungua miaka 600 iliyopita.

Karagwe ikiwa ni miongoni mwa sehemu chache za Tanzania ana Afrika ya Mashariki ambayo historia yake imendikwa tangu hata kabla ya ukoloni, yataoneshewa machapisho mbali mbali yanayoitunza historia ya Karagwe.
Baadhi ya malikale zitakazooneshea ni zana za chuma zilizotengenezwa Karagwe kwa zaidi ya maiaka 400 iliyopita kwa teknolojia ambayo haikuwa imefikiwa na hata baadhi ya mataifa ya Ulaya.

Karibu sana Nyakahanga shule ya msingi uone utamaduni wako.
Mawasilianao
Bullet Ruhinda 0754030242
Frontline Ruhinda 0757026908

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top