Hatimaye uchaguzi wa Meya wa jiji la
Dar es Salaam umekamilika leo katika ukumbi wa Karimjee, na kushuhudia Isaya
Mwita wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitangazwa kuwa
mshindi wa uchaguzi huo.
Mwita ameibuka na ushindi na kutangazwa kuwa Meya Mpya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kupata kura 84 akimshinda mpinzani wake, Yenga Omary wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 67.
Post a Comment