Kamati
ya bunge ya huduma za jamii imeitaka Wizara ya Afya ijieleze ndani ya siku saba
kwanini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, aliwasimamisha watumishi wa Afya wa
hospitali ya Butimba bila kufuata hatua stahili.
Mapema
mwezi huu, Magesa Mulongo aliwasimamisha kazi madaktari 3, manesi 6, na
wafanyakazi wengine 2 wa hospitali ya Butimba kwa madai mbalimbali, yakihusisha
kifo cha watoto mapacha. Lakini Mulongo alijitetea maamuzi yake kuwasimamisha,
akisema ilitokana na tendo walilofanya kutoendana na sheria za kazi.
Mwenyekiti
wa kamati Raphael Chegeni, alisema kamati iligundua kwamba kulikuwa na matumizi
mabaya ya madaraka katika maamuzi ya mkuu wa mkoa. Na kwamba mkuu wa mkoa
hakuomba taarifa ya utenda kazi ili kutambua matatizo ya hospitali.
Mmoja
wa wanakamati Mhe. Zitto Kabwe ndiye aliuliza ni kitu gani hasa
kilichosababisha mkuu wa mkoa kusimamisha watumishi hao, kwani kuna wagonjwa wengi wanaofariki katika
hospitali husika kwa kukosa tiba na wengine wakiwa na shida mbalimbali.
Raphael
Chegeni alisema mkuu wa mkoa hakufuata kanuni, zinazohitaji watumishi wa afya
kusimamishwa na mabaraza yao.
Kamati
imejiridhisha kwamba mkuu wa mkoa aliwasimamisha wafanyakazi hawa wa afya kwa
kutumia nguvu ya kisiasa" alisema Raphael Chegeni. Pia alionya wanasiasa,
kuchanganya siasa na utoaji wa huduma za afya, hususani maeneo ya vijijini,
kwani mwisho wa siku itawaamiza wakaazi wa vijijini.
Akichangia,
mbunge wa viti maalumu Mhe. Suzan Lyimo alisema viongozi wa serikali wanapaswa
kutambua mchango wa watumishi wa afya wanaofanya kazi kubwa kuokoa maisha.
Kamati
pia ilishauri wizara kuboresha mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa afya, ikiwa
ni pamoja na kuboresha mishahara na marupurupu.
Post a Comment