Shirikisho
la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (sawa na
Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la
kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber)
ya shirikisho hilo.
Kamati
ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc
500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama
za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.
Simba
imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Mosoti Omanua kwa wakati tangu
mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa
alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola
29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh
1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia
Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya
kusimamia kesi hiyo.
Felix
Majani, Mwanasheria wa Mosoti, ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa FIFA,
alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka makubaliano
ya mkataba na mteja wake.
Kwa
kosa hilo Simba inatakiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha ndani ya siku
30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu
na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016. TFF imekuwa nakala na maagizo kuisimamia
Simba inalipa kiasi hicho cha fedha.
Simba
imeagizwa kulipa stahiki zote za Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya
kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo
Mei 6, 2016.
Katika
barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kuhakikisha
inalipa na isipotekeleza agizo hilo mara moja itakatwa pointi tatu katika mechi
zake Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara –VPL.
FIFA
imekwenda mbali zaidi ikisema ikiwa klabu hiyo kama haitalipa katika muda
uliopangwa yaani siku 30 kutoka sasa, FIFA itaishusha Simba daraja kutoka Ligi
Kuu Tanzania Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.
Kwa
upande wake, TFF imagizwa kuhakikisha uamuzi huo unasimamiwa vema utekelezwaji
wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwamo kuiondoa Tanzania
katika mashindano ya kimataifa.


Post a Comment