Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE YAPATA GARI LA ZIMAMOTO
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Halmashauri   ya   wilaya   ya   Karagwe   Mkoani   Kagera   imefanikiwa   kupata   gari   la   zimamoto   na   linatarajiwa   ...





Halmashauri  ya  wilaya  ya  Karagwe  Mkoani  Kagera  imefanikiwa  kupata  gari  la  zimamoto  na  linatarajiwa  kufika  wilayani  humu  ndani  ya  wiki  moja  hii  inaifanya  wilaya  ya  karagwe  kuwa  miongoni  mwa  halmashauri  chache  hapa  nchini  kuwa  na  gari  la  zimamoto.

Akizungumza kwa  nia  ya  simu  kutoka  mjini  Dodoma  anakohudhuria  vikao  vya  Bunge  vinavyoendelea  Mbunge  wa  Jimbo  la Karagwe  Innocent  Bashungwa  amesema  gari  hilo  tayari  limepatikana  hivyo  wananchi  wa  wilaya  ya  Karagwe waondoe  shaka  juu  ya  kutokuwepo  gari  la  Zimamoto.

Bashungwa  amesema  anaishukuru  serikali  kuwa  sikivu  kwa  kukubali  ushauri  na  maombi  ya  wilaya  yaliyowasilishwa  na  kuongeza  kuwa  anampongeza  pia   mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe  kwa  Deodatus  Kinawiro  kwa  ushirikiano  wake  alioutoa  katika  kufanikisha  kupatikana  kwa  gari  hilo.



Amesema  halmashauri  nyingi  hazina  magari  ya  zimamoto  maana  ni  ghali  mno  kuzipata  na  kwa  wilaya  ya  Karagwe  wametumia  ushawishi  mkubwa  wa  kuelezea  kukua  kwa  kasi  mji  wa  Kayanga  na  uwepo  wa  viwanda  vya  kukoboa  kahawa  pia  kutokana  na  majanga  ya  moto  na  hiyo imesaidia  kujenga  usawishi  wa  kuhakikisha  kupata  gari  hilo.

Aidha  Bashungwa  amesema  changamoto  nyingine  zinazoikabili  wilaya  ya  Karagwe  ataendelea  kuziwasilisha  serikalini  pia kuishauri  kuiangalia  Karagwe  kwa  jicho  la  pekee.

Hata  hivyo  amewataka  wananchi  wote  katika  jimbo  la  Karagwe  kuendelea  kufuatilia  na  kutumia  ushauri  unaotolewa  na  watalaamu  ili  kuweza  kuepuka  majanga  yasiyokuwa  ya  lazima.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top