Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaaf SALUMU KIJUU amesema kuwa
atawachukulia hatua wafanyabiashara wote ambao wataenda kinyume na bei ya
sukari iliyotolewa na serikali.
Akizungumza na vyombo vya habari
KIJUU amesema atasita kuwachukulia hatua wale woteambao watajipangia bei ya
sukari na kwenda na bei elekezi kutokana na kiwanda cha sukari cha kagera
sukari kuacha kuzalisha sukari katika kipindi hiki cha mvua.
Amefafanua kuwa kutokana na kumuzuia
wakala wa kusambazasukari kuacha kusambaza sukari katika mikoa ya jirani
wananchi wanapaswa kutoa taarifa kupitia kamati ya ulinzi na usalama kama
kutakuwepo na utoroshwaji wa sukari nyakati za usiku kwenda katika mikoa hiyo.
Aidha ametaja vigezo vilivyotumika
kutambua maduka matatu matatu kila kata ya wafanyabiashara ambao watauza sukari
kwa bei elekezi.
Hata hivyo Meja Jeneral
Mstaafu KIJUU amesema kuwa sukari itarejea katika khali ya kawadaida mwezi wa
sita ambapo sukari itaendelea kusambazwa katika mikoa jirani .
Post a Comment