MSIBA
MZITO CAMEROON.....DOOH
Mchezaji wa timu ya taifa ya Cameroon Patrick
Ekeng ( 26) amefariki dunia jana akitokea benchi na timu yake ya Dinamo
Bucharest nchini Romania .
Patrick aliingia kipindi cha pili akicheza
kama kiungo wa chini lakini ghafla dakika ya 70 akiwa peke yake alianguka
ghafla na kufariki .
Patrick aliyejiunga na timu hiyo january hii
ametonesha msiba wa taifa hilo , Africa na familia ya wapenda soka duniani
kukumbuka kifo kama hicho cha gwiji la soka Marc Vivien Foe mwaka 2003 ambaye
naye alifariki uwanjani ghafla na akicheza nafasi hiyo hiyo.
Jiji la Younde na viunga vyake limezizima
kwa huzuni kubwa .


Post a Comment