Watumishi wametakiwa
kufanya kazi kwa uadilifu,uwajibikaji na
kujituma zaidi ili
kuwatumikia wananchi na
wala watumishi wasijione wao
ni maboss wamepewa dhamana
hiyo kuwatumikia wananchi
kwa ajili ya
kutatua kero zao.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Salum
Mustapha Kijuu wakati
akiongea na watumishi
wa kada mbalimbali wa
halmashauri ya Karagwe
hiyo ikiwa ni
ziara ya kujitambulisha tangu
kuteuliwa na Rais
wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
Dk Jih Pombe Magufuli.
Amesema kuwa
zama za kutegea
kazi,kufanya kwa uzembe
na kulindana imepitwa
na wakati sasa
ni awamu ya
kazi tu hivyo watumishi watambue
hilo na wakizingatia
uwajibikaji na uadilifu
zaidi na atakayeshindwa kuzingatia
hayo hawatasita kumuondoa
kwenye nafasi hiyo
mara moja.
Mkuu wa
Mkoa Kijuu amesetoa maagizo ambayo
amesema kuwa yatakuwa
ni kipimo cha
utekelezaji wa kazi kwa kila
halmashauri hapa mkoani
Kagera kwa kipindi
cha kuanzia mwezi
huu huku akisisitiza
suala la ukusanyaji
mapato kupewa kipaombele
kikubwa zaidi huku
akionya wanaokusanya mapato
bila kufikisha pesa
benki.
Ametoa muda
wa siku 14
za kuhakikisha uongozi
wa halmashauri kufanya uthamini
wa majengo kwa ajili
ya kupanga kiwango
cha ulipaji kodi
ya majengo kwani
ni chanzo muhimu
cha kuingizia halmashauri
na serikali mapato pia
ameagiza makusanyo yote
ya kodi ya
halmashauri utumie mfumo
wa kielectroniki yaani
EFDs kuanzia mwezi
juni
Aidha agizo
jingine ni utekelezaji
wa maagizo ya
serikali kwa wakati
na halmashauri ambayo
haitimiza mikutano ya
kisheria itawajibishwa na
kutoa taarifa zisizokuwa
sahihi hazitavumiliwa .
Meja Jenerali
Kijuu ameagiza pia
taarifa ya mkaguzi
na mdhibiti wa
hesabu za serikali
CAG zitolewe siku
21 zikiwa na viambatanisho
vyote vinavyohitajika ili
kuweza kuepuka kupata
hati zenye mashaka
au chafu.
Katika usimamizi
wa shughuli za
serikali amemtaka mkurugenzi
na idara ya
ujenzi kuweka wazi
maelezo ya mradi
unaanza lini unatarajia
kuisha lina pia gharama
za mradi huo
zianishwe na mkandarasi
ni nani anayetekeleza mradi
huo.
Hata hivyo
ameutaka uongozi wa
halmashauri ya wilaya
ya Karagwe kukuna
vichwa kwa ajili
ya kutenga maeneo
ya kuwawezesha vijana
kufanya kazi kuliko
kuendelea kuzurula na kusema
hilo atalifuatilia kwa
karibu.
Post a Comment