Jumla
ya wanachama 12 wameangukia pua katika kuwania nafasi za ujumbe wa kamati ya
utendaji ya klabu ya Yanga katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliomalizika
rasmi asubuhi ya leo.
Zoezi
la uchaguzi lililazimika kumalizika leo hii alfajiri kutokana na kuchelewa kwa
uhesabu wa kura za nafasi mbalimbali zilizowania.
Yusuph
Manji alifanikiwa kutetea nafasi yake ya mwenyeti baada ya kupata kura 1468
kati ya 1470 zilizopigwa huku kura mbili zikiharibika
Waliofanikiwa
kushinda nafasi nane za ujumbe ni Siza Lymo(1027), Omary Said Amiry(1069),
Tobias Lingalangala (889), Salim Mkemi(894), Ayoub Nyenzi(889), Samuel Lukumay
(818), Hashim Abdallah (727) na Hussein Nyika kura 770
Wagombea
waliochemka ni David Luhago aliyepata kura 582, Godfrey Mheluka (430), ramadhan
kampira(182), Edgar Chibura(72), Mchafu Chakoma(69), George Manyama (249), bakari
malima (577), Lameck Nyambaya(655), Beda Tindwa(452), Athuman Kihamia (558),
Paschal Laizer(178) na Silvester Haule (197)
Post a Comment