Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe anatarajia
kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kagera kuanzia tarehe 14-16 Julai,
2016.
Siku ya kwanza ya tarehe 14 Julai, 2016 Mwakyembe anatarajia kukutana na kuongea na wadau waliopo chini ya Wizara yake ya
Sheria na Katiba pamoja na Vyombo vya Habari katika Ukumbimbi wa Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Kagera kuanzia saa 6:00 hadi saa 7:00 Mchana. Aidha kuanzia saa 7:30
hadi 8:30 mchana atatembelea ofisi za RITA kujionea uandikishaji wa watoto
waliochini ya miaka mitano.
Katika siku ya pili ya tarehe 15 Julai, 2016 Mwakyembe
atatembelea Gereza la Wafungwa la Mkoa wa Kagera, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba
na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Manispaa ya Bukoba ili kuongea
na uongozi wa ofisi hizo ambazo zipo chini ya Wizara yake.
Siku ya tatu ya tarehe 16 Julai, 2016 Mwakyembe akiwa
mkoani Kagera ataelekea Wilayani Biharamulo ambapo atatembelea Gereza la
Wafungwa Biharamulo na kuhitimisha ziara yake katika Mkoa wa Kagera na kuondoka
kuelekea Mkoani Mwanza.
WAKATI
HUO HUO Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee, na Watoto Ummy Mwalim anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili
Mkoani Kagera kuanzia tarehe 15-16 Julai, 2016.
Katika
ziara hiyo Ummy Mwalim anatarajia kuzindua wodi ya wazazi katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Kagera kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana siku ya
Ijumaa tarehe 15 Julai, 2016. Mara baada ya uzinduzi wa wodi ya wazazi katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Waziri ataelekea Wilayani Muleba kutembelea
Hospitali Teule ya Wilaya ya Rubya.
Katika
siku yake ya pili Mkaoni Kagera tarehe 16 Julai, 2016 Ummy Mwalim atatembelea
kituo cha kuwatunza wazee Kiilima kilichopo Wilyani Bukoba kuanzia saa 4:00
asubuhi. Kituo hicho cha Kiilima kipo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto ambapo kwasasa kinawatunza wazee 18 wanaume
wakiwa 14 na wanawake 4 pamoja na watoto yatima10.
Wito
kwa wananchi wote hususani wanawake wanaombwa kuhudhuria kwa wingi hasa kwenye
uzinduzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera
kushuhudia Waziri akizindua wodi ya wazazi ambapo mara baada ya uzinduzi wa
wodi hiyo huduma kwa wazazi zitaimarika zaidi na kupunguza msongamano kwa kiasi
kikubwa katika wodi ya wazazi ya zamani.
Post a Comment