Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WAZIRI UMMY MWALIMU KUTEMBELEA MKOA WA KAGERA KUANZIA TAREHE 15 HADI 16 MWEZI HUU
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA Anwani ya Simu: “REGCOM” Simu ya ...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA


Anwani ya Simu: “REGCOM”
Simu ya mdomo: (028) 2220215-18
Fax: (028) 2222341 / 2221356
OFISI YA MKUU WA MKOA,
S. L. P. 299,
BUKOBA - KAGERA.
TANZANIA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 11 JULAI, 2O16

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalim anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera kuanzia tarehe 15-16 Julai, 2016.

Katika ziara hiyo Mhe. Ummy Mwalim anatarajia kuzindua wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana siku ya Ijumaa tarehe 15 Julai, 2016. Mara baada ya uzinduzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mhe. Waziri ataelekea Wilayani Muleba kutembelea Hospitali Teule ya Wilaya ya Rubya.

Katika siku yake ya pili Mkaoni Kagera tarehe 16 Julai, 2016 Mhe. Ummy Mwalim atatembelea kituo cha kuwatunza wazee Kiilima kilichopo Wilyani Bukoba kuanzia saa 4:00 asubuhi. Kituo hicho cha Kiilima kipo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto ambapo kwasasa kinawatunza wazee 18 wanaume wakiwa 14 na wanawake 4 pamoja na watoto yatima10.

Wito kwa wananchi wote hususani wanawake wanaombwa kuhudhuria kwa wingi hasa kwenye uzinduzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kushuhudia Mhe. Waziri akizindua wodi ya wazazi ambapo mara baada ya uzinduzi wa wodi hiyo huduma kwa wazazi zitaimarika zaidi na kupunguza msongamano kwa kiasi kikubwa katika wodi ya wazazi ya zamani.


Sylvester Raphael
Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

11 Julai, 2016

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top