WATU
11 wamekufa papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa katika ajali mbili
tofauti zilizotokea sehemu moja, zikihusisha basi la abiria, lililopamia
malori mawili ya mizigo yaliyogongana uso kwa uso na kuungua moto eneo
la Dakawa – Veta, wilayani Kilosa.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema mjini hapa jana
kuwa ajali ya kwanza, malori mawili ya mizigo yaligongana uso kwa uso
juzi saa 12 jioni na kuwaka moto.
Katika
ajali hiyo ya juzi jioni, lori la mizigo aina ya Scania ambalo namba za
mbele hazikutambuliwa, lakini tela lake ni namba T 704 CEC, likitoka
Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kanda ya Ziwa, liligongana uso kwa uso na
lori aina ya Fuso yenye namba za usajili T 963 BLW, lililokuwa likitokea
Dodoma kwenda Dar es Salaam.
Kamanda
Matei alisema katika ajali hiyo, watu watano walipoteza maisha papo
hapo kwa kuungua moto mpaka ikashindikana kuwatambua, akiwemo dereva wa
bodaboda aliyekuwa pembeni mwa barabara na pikipiki yake katika eneo la
tukio.
Wengine
waliokufa papo hapo na kushindwa kutambulika kwa mujibu wa Kamanda
Matei, ni madereva wa malari hayo na wasaidizi wao wawili; mmoja kwa
kila lori.
Alisema
chanzo cha ajali hiyo, ni kutokana na gari ndogo iliyokuwa mbele ya
Fuso hilo kusimama ghafla na kusababisha dereva wa Fuso kupita pembeni
bila kuangalia mbele na kugongana uso kwa uso na Scania yenye shehena ya
mafuta na kusababisha malori hayo kuwaka moto.
Wakati
malori hayo yakiwa eneo la tukio, jana alfajiri kulitokea ajali
nyingine ambapo basi la abiria mali ya Kampuni ya Otta Classic yenye
namba za usajili T 201 DGK aina ya Higer, liliparamia moja ya malori
yaliyokuwa yamepata ajali katika eneo hilo na kuua watu sita papo hapo
na kujeruhi wengine 44.
Kamanda
Matei alisema kati ya majeruhi hao, sita hali zao ni mbaya na
walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro kupatiwa matibabu
zaidi. Alisema ajali hiyo ilitokea saa 10 alfajiri ya Julai Mosi mwaka
huu, wakati basi hilo likitokea Bukoba mkoani Kagera kwenda Dar es
Salaam.
Waliokufa
katika ajali hiyo kwa mujibu wa Kamanda Matei ni dereva wa basi hilo,
msaidizi wake, kondakta na abiria wengine watatu.
Alitaja
majina ya waliokufa kuwa ni Yassin Mgongolwa (41) dereva wa basi hilo,
Veronica Jeremia ambaye ni kondakta, Said Shomari Simba (30) dereva
msaidizi na abiria Lilian Paul (34), Jonia Kokumbuga na mwamamke
mwingine mwenye umri kati ya miaka 30 -35, ambaye hajatambulika.
Miili
ya marehemu hao na maiti zilizoungua na kushindwa kutambuliwa,
imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.
Kamanda
Matei alisema kabla ya basi hilo kupata ajali, lilisimamishwa na askari
wa usalama barabarani, lakini dereva alikaidi na kupitiliza na baada ya
muda likapata ajali hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe, ambaye pia alifika eneo la tukio
hilo jana, alisema miili iliyoungua, itatambuliwa kwa kutumia vinasaba
(DNA) na kuwataka ndugu na jamaa zao kuwa na subira wakati utambuzi huo
utakapofanyika.
Alilipongeza
Jeshi la Polisi mkoa na vikosi vya Zimamoto na wananchi wa vijiji vya
karibu na eneo la ajali kwa kusaidia kuzima moto na kuokoa majeruhi wa
ajali hiyo.
Gari la OTA HIGH CLASS lililokuwa likitokea BUKOBA kuelekea Jijini DAR ES SALAAM limepata ajali eneo la KILOSA mkoani Morogoro baada ya kugongana na lori taarifa za awali zinaeleza kuwa dereva na wahudumu wa Bus wote wamepoteza maisha pamoja na abiria wawili huku amajeruhi wakiwa 15 habari zaidi tutaendelea kuwajuza kadri takavyozipata.
Mungu awape uvumilivu ndugu jamaa na watanzania wote kwa msiba huu.
Post a Comment