Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA TAMKO CHAITAKA SERIKALI KUHESHIMU HAKI ZA WATANZANIA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Serikali imetakiwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kuwapa wananchi habari na taarifa muhimu zinazowahusu bila ya kujali gharama za taar...
Serikali imetakiwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kuwapa wananchi habari na taarifa muhimu zinazowahusu bila ya kujali gharama za taarifa hizo kwa kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na kituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake Bi. Imelda Urio na kuongeza kuwa kusitishwa baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kwa kisingizio cha gharama ni kitendo cha makusudi kwa kuwanyima wananchi taarifa muhimu toka kwa wawakilishi wao ambao ni wabunge.

Bi Imelda Urio ameongeza kuwa muhimili wa bunge na viongozi wake lazima wafanye kazi kiueledi na kuzuia mianya ya kuingiliwa na mihimili mingine hususani serikali.

Aidha LHRC imelaani vikali kitengo cha kuzalilishwa kwa wabunge kwa kutolewa bungeni na mbwa wa jeshi la polisi,

Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa utetezi na maboresho Bi. Anna Henga yeye amesema kuwa haki yoyote haina gharama na ni jukumu la serikali kulipia gharama hizo za matangazo ya bunge.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top