Mbunge
wa Viti Maalumu Chadema, Jesca Kishoa, amehoji kwa nini Tasisi ya
Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema watu 36 watafikishwa mahakamani
kwa tuhuma za ufisadi lakini vinara wa kashfa ya Tegeta Escrow, ikiwa ni
pamoja na Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habirnder Seth
Singh, hayumo.
Kishowa
ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye
aliishupalia hoja hiyo bungeni na kuwang’oa baadhi ya vigogo wa serikali
wakiwemo mawaziri.
Kafulila
ndiye Mbunge wa kwanza kuifikisha kashfa hiyo kwenye Bungeni la 10 na
baadaye Ofisi ya Mdhimiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
ikafanya uchunguzi na kuwasilisha ripoti yake ambayo ilifikishwa Bungeni
na Kamati ya Hesabu za Serikali.
Kashfa
hiyo ilisababisha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka kuachia ngazi.
Watumishi
wengine walioguswa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema,
Wenyeviti wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, Kamati ya
Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja na Kamati ya Bajeti, Andrew
Chenge.
Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alikumbwa na fagio hilo.
Kwenye
mkutano wa jana wa Bunge, Kishowa alitaka kupewa maelezo kwa nini
mmliki huyo wa IPTL hajachukuliwa hatua na kusema hata baadhi ya
maazimio ya Bunge yaliyopitishwa hayajafanyiwa kazi.
Alisema
ingawa anajua Mwenyekiti aliyekuwa akiongoza kikao cha jana, Chenge,
ana maslahi katika suala hilo ni vyema akatoa mwongozo wa kiti.
Akijibu mwongozo huo, Chenge alisema, limeulizwa sehemu ambapo siyo kabisa.
Post a Comment