Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WANANCHI MKOANI KAGERA WATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi mkoani KAGERA  wenye kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea walioajiriwa katika sekta rasmi na zisizo rasmi wameshauriwa kujiung...

Wananchi mkoani KAGERA  wenye kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea walioajiriwa katika sekta rasmi na zisizo rasmi wameshauriwa kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF ili kupata huduma mbalibali za jamii.

Akizungumza na KARAGWE FORUM  afisa mfawidhi wa mfuko wa PSPF mkoa wa KAGERA CHRISTIAN MWAIPOPO amesema kuwa mfuko huu  ni wa  hiari unawahusu wananchi wote ambao wako tayari kujiunga na mfuko huu wa hifadhi ya jamii

.
Mwaipopo amesema kuwa kutokana na PSPF kuanzisha mfuko wa hiari kwa wananchi wote wanaotaka kujiunga  toka mwaka 2011 licha ya manufaa wanayoyapata kutokana na kujiunga katika mfuko huo suala la afya linapewa sana kipaumbele.


Amefafanua kuwa kama mwananchi amejiunga na akataka kujiondoa katika mfuko huo anapewa stahiki zake zote huku akibainisha kuwa kwa wale wanaolipia zaidi ya miaka 15 wanapewa fidia.

Akizungumzia sekta binafsi kujiunga katika mfuko huo amesema kuwa ,mwajiriwa wa sekta binafsi endapo atajiunga na kufuata masharti na kanuni zilizowekwa na mfuko huo atapatiwa huduma kama mwajiriwa wa serikali.

.
Aidha MWAIPOPO ametoa wito kwa wananchi ambao hawajajiunga katika mfuko wa hiari huku akiwaomba wale waliojiunga kufika mara kwa mara katika ofisi za PSPF kukagua taarifa zao za michango na kupata elimu mbalimbali.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top