Rais
Magufuli aliyaeleza hayo jana katika hotuba yake kwa mabalozi mbalimbali
wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania iliyosomwa kwa niaba yake na
waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na
kimataifa Balozi Augustine Mahiga jana ikulu jijini Dar es salaam.
Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli aliwaeleza mabalozi hao kuwa licha
ya Tanzania kuwa nchi moja, Zanzibar ina mfumo wake wa siasa, ina
serikali yake, Katiba yake na pia tume yake ya uchaguzi inayojitegemea.
Alisema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu
yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi
wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.
Alosema mazungumzo ya kutatua mgogoro huo yalifanyika bila mafanikio
ambapo chama kikuu cha upinzani (CUF) kimeendelea kupinga uchaguzi wa
marudio huku vyama vingine kikiwemo chama tawala vikionesha uhitaji wa
uchaguzi huo wa marudio.
Alisema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo,
na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa
kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.
Aliwaeleza mabalozi hao kuwa serikali pamoja na watanzania walio
wengi wangependa kuona CUF inathibitisha madai yake ya kushinda uchaguzi
huo kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa marudio.
“Tunakiasa chama cha CUF kama ambavyo watanzania wengi wangependa
kuona, kuthibitisha madai ya ushindi wao katika sanduku la kura, hakuna
jinsi nyingine ya kutatua suala hili zaidi ya kukubali kufanya uchaguzi
wa marudio” ilisema sehemu ya hotuba hiyo.
Magufuli amewahakikishia mabalozi hao kuwa nchi ni salama na hali ya
amani na utulivu ni ya kuridhisha katika kipindi hiki cha kuelekea
katika uchaguzi wa marudio.
Post a Comment