Siku
chache baada ya kutokea tukio la majangili katika pori la akiba Maswa
wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, kuitungua ndege (helikopta) iliyokuwa
doria na kuaawa kwa rubani wake Rodgers Gower (37), watu 9 wamekamatwa
kuhusika na tukio hilo.
Katika watuhumiwa hao mmoja ni Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kitengo cha Interejensia, ambaye alitajwa kuwa mhusika Mkuu wa kufanikisha tukio hilo sambamba na kukamatwa mganga wa jadi.
Akitoa
taarifa mbele za waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa
polisi Mkoani Simiyu Lazaro Mambosasa alisema kuwa kukamatwa kwa
watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kufanya kazu usiku na mchana
kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA.
Kamanda
Mambosasa alisema watuhumiwa wote walikamatwa na kukiri kuhusika na
tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa uliofanywa na jeshi hilo
mara baada ya tukio kutokea chini ya Mkuu wa upelelezi Mkoa Jonathan
Shana.
Alisema
katika msako huo baadhi ya watuhumiwa walibainika kuwa kiungo kikubwa
kufanikisha tukio hilo kwa kutoa mbinu za uharifu, huku wakijihusisha na
matukio ya ujangili kwa muda mrefu.
Aliongeza
kuwa baadhi yao walibainika kuwa waganga wa jadi, ambapo walikuwa
wakitoa dawa kwa majangili za kuosha silaha, ikiwa ni pamoja na kuosha
na kusafisha miili yao ili wasiweze kukamatwa.
Mambosasa
aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shija Mjika (38), Njile Gonga (28)
Mhazabe, Masasi Mandago (48) pamoja na Dotto Pangali (41) , ambao ndio
walihusika kutungua helkopta hiyo.
Wengine ni Iddi Mashaka (49) ambaye Kamanda Mambosasa alimtaja kuwa Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro Kitengo cha Intelijensia na ndiye alikuwa kiungo Mkuu wa tukio hilo.
Aliwataja
wengine kuwa ni Mapolu Njige (50) ambaye ni mganga wa jadi aiyekuwa
anatumika kutoa dawa za kutokamatwa kwa majangili hao, Mwigulu Kanga
(40) , Dotto Huya (45) , Pamoja na Mange Balumu.
Aidha
Mambosasa alisema kuwa Mtuhumiwa Dotto Pangali alikamatiwa katika
wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga mnamo tarehe 7/02/216 na kufanyiwa
upekuzi nyumbani kwake ambapo alikutwa na bunduki aina ya Riffle yenye
namba .7209460 CAR Na.63229.
Mkuu
huyo wa polisi alisema Mtuhumiwa huyo alikiri bunduki hiyo kutumika
katika tukio la kuuawa kwa rubani huyo, ambapo ilibainika kuwa bunduki
hiyo inamilikiwa na Mange Magima ambaye pia amekamatwa.
Alisema
msako uliendelea nyumbani kwa Pangali na kufanikiwa kukamatwa kwa
bunduki nyingine aina ya Riffle Na3478 CAR 458 ikiwa na risasi 6 ambayo
ilibainika kumilikiwa na Nghomango Jilala ambaye mpaka sasa hajakamatwa.
Alieleza
kuwa jeshi hilo liliendelea kupata taarifa ambapo mnamo tarehe
29/01/2016 walikamatwa Shija Mjika, Njile Gonga, pamoja na Masasi
Mandago wakiwa na meno ya tembo 2 yakiwa na uzito wa Kilo 31 yakiwa
yamefichwa chini ya daraja katika kijiji cha Itaba.
Aidha
Mambosasa alieleza kuwa baada ya kukamatwa kwa wahusika wote ilibainika
kuwa bunduki zilizotumika katika tukio hilo zinamilikiwa kihalali na
watu ambao waliomba kuzimiliki kwa ajili kujilinda.
“Mbali
na tukio hilo bunduki nyingi wamiliki wake wanawaazimisha majangili kwa
ajili ya kutumika kwa uhalifu pamoja na kuua wanyama ndani ya
hifadhi…lakini na hao wamiliki wanalipwa pesa baada ya uhalifu
kufanyika” ,alisema.
Alisema
baada ya kubaini hilo kulifanyika msako mwingine kwa wanaomiliki
silaha, ambapo alisema asilimia kubwa wanaishi karibu na hifadhi, na
jumla ya bunduki 27 zimekamatwa na mara baada ya uchunguzi wamiliki
watarudishiwa.
“Tunajiandaa
kupeleka zuio la silaha mahakamani ili kubaini kama wana sifa za
umiliki…lakini mbali na hilo sasa kutaanzishwa oparesheni kwa watu wote
wanaomiliki silaha hasa maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kuwanyanganya”, alisema.
Mkuu
huyo wa polisi alisema kuwa upelelezi juu ya tukio hilo umekamilika na
watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani leo Jumanne ili kujibu tuhuma
zinazowakabili, ambapo alioomba mahakama kuharakisha hukumu kwa vile
uchunguzi umekamilika.
Kwa
upande wake Mhifadhi mkuu wa Serengeti William Mwakilema amelipongeza
jeshi la polisi ambapo amesema tukio hilo lilipotokea liliwasikitisha
sana kwani hasara ilipatikana kutokana na kutunguliwa kwa helkopta.
Mnamo
tarehe 29/01/2016 saa 11:30 jioni katika eneo la Gululu lililopo ndani
ya hifadhi ya Maswa kata ya Mwangudo wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu,
majangili waliipiga risasi ndege (helkopta) 88HFCG iliyokuwa doria na
kusababisha kifo cha rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza
huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika
kifo.
Post a Comment