Baada ya mamulaka ya mawasiliano tanzania [TCRA] kutoa semina
kuhusu uzimaji wa wa simu bandia baadhi ya mafundi simu na
wafanyabiashara wa simu wamekuwa na maoni tofauti tofauti kuhusiana na uzimaji
wa sm hizo.
Wamesema kuwa wanakubariana na mamuzi ya mamlaka ya mawasiliano TCRA ingawa mpaka sasa wanabidhaa nyingi ambazo pengine ni bandia au sio bandia.
Wamesema kuwa wanakubariana na mamuzi ya mamlaka ya mawasiliano TCRA ingawa mpaka sasa wanabidhaa nyingi ambazo pengine ni bandia au sio bandia.
Comission msaidizi wa jeshi la polisi mkoani KAGERA amesema kuwa uzimaji wa simu bandia unamanufaa makubwa kwa jeshi la polisi hivyo nivizuri zikazimwa kama serikali ilivyopangwa.
Amebainisha kuwa kama simu bandia zitazimwa kutakuwepo na manufaa makubwa kwani kulingana na idadi kubwa ya watumia simu kuongezeka tayari vitendo vya huarifu vinaongezeka siku hadi siku kwani simu bandia zikizimwa kila mmiliki wa simu atajulikana.
Aidha msaidizi wa jeshi la polisi hakusita kutaja changamoto zitakazolikabili jeshi la polisi baada ya simu hizo kuzimwa na kuongeza kuwa licha ya jeshi la polisi kuwa na mbinu nyingi bado na waharifu wanajifunza mbinu mpya.
Zoezi la kuzima sm bandia litafanyika Juni16 mwaka huu kote nchini ili kuwawezesha wananchi kutumia sm zao vizuri na kuepuka usumbufu unaojitokeza mara kwa mara.
Post a Comment