Wakulima
wa zao la kahawa mkoa wa Kagera wametofautiana na serikali ya mkoa huo ,baada
ya kuitaka seikali kutoa fulsa ya kuuza kawaha sehemu yoyote kutokana na
kushindwa kudhibiti ubora wa bei ya kahawa,uku kahawa nyingi ikielezwa
kusafirishwa kwa njia ya magendo kuuzwa Uganda.
Meya
wa Manispaa ya Bukoba Chifu Kalumuna ambaye haoni umuhimu wa serikali
kuwaingilia wakulima wa zao la kahawa katika biashara ya uuzaji wa zao
hilo pindi wakulima wanapovuna.
Katika
kikao cha bodi ya kahawa mkoa wa Kagera kilichowahusisha ,viongozi wa serikali
kutoka kila halmashauri na wakulima ,ambapo wakulima wa zao hilo
wanaeleza ugumu wa kudhibiti kahawa kuuzwa kwa magendo.
Baada
ya majadiriano ya muda mrefu mkuu wa mkoa wa kagera Meja Jenerali Mstaafu
SALUM KIJUU anapiga marufuku magendo ya kahawa na kuahidi kuwachukulia hatua
kali watakaobainika ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi.
Zao
la kahawa usafirishwa kwa njia ya magendo kwenda nchini Uganda kupitia mipaka
ya Murongo na Mtukula wilayani Missenyi.



Post a Comment