Mbeki Mbeki, Karagwe
FEDHA alizolipwa meneja
miradi katika kampuni ya MG contractor ya jijini Mwanza aliyekuwa mkandarasi
wa ujenzi wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa mpunga
Mwisa Kijiji cha Bujuruga wilayani Karagwe zimeonekana kuwa tofauti
ikilinganishwa na kiasi cha fedha kilichotajwa na mwakilishi wa halmashauri
hiyo baada ya mkandarasi huyo kuonyesha tofauti ya kiasi cha
shilingi 53 milioni.
Hayo yalibainika jana katika
makabidhiano ya Mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa kilimo cha mpunga Mwisa
kijiji cha Bujuruga kata ya Bugene wilayani humo ambapo mradi
huo ulikabidhiwa kwa wananchi hao na Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Karagwe Wallesi Mashanda ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika mkutano huo wa kukabidhi mradi ambao ulikuwa unasimamiwa
na halmashauri ya wilaya ya Karagwe pamoja na Idara ya umwagiliaji
kanda kutoka jijini Mwanza richa ya kuwepo kamati ya usimamizi wa
mradi katika kijiji hicho.
Ofisa kilimo katika halmashauri ya
wilaya ya Karagwe Adamu Salumu alisema kwamba, kazi zote zilizofanyika thamani
yake ni shilingi 433, 226 616.28 milioni na
mkandarasi alilipwa milioni 352, 961, 560.63 gharama ya mkataba
ilikuwa ni shilingi 586, 037,278 milioni na kuwa kutokana na
kutokamilika kwa mradi huo tayari wameomba kiasi cha
shilingili 185 milioni kutoka shirika la Japan lijulikanalo kama
JAIKA fedha ambazo zitasaidia kukamilisha mradi.
Kwa upande wa meneja wa kampuni
miradi katika kampuni ya MG contractor kutoka jijini
Mwanza mhandisi Jumanne R. Werema alisema kuwa, hakubaliani
na kiasi kilichotajwa na mwakilishi kutoka halmashauri ya wilaya
hiyo ambaye ni ofisa kilimo badala yake yeye mpaka sasa ameisha pewa kiasi cha
shilingi 289 milioni.
“Ukweli ni kwamba mpaka sasa
kampuni ninayoisimamia imeisha pokea kiasi cha shilingi milioni 289 tofauti na
msemaji wa halmashauri ya wilaya alivyosema kuwa nimeisha pokea kiasi cha
shilingi 352.9 milioni kama ni hivyo mkurugenzi huyo ni jipu linalofaa
kutumbuliwa” Alisema mhandisi Werema.
Aidha Wananchi wa kijiji cha
Bujuruga kata ya Bugene wilayani Karagwe wamekabidhiwa mradi wao wa
kilimo cha umwagiliaji wa mpunga Mwisa huku wananchi hao wakionekana
kutofautiana baadhi wakikataa kupokea mradi kwa kigezo kuwa mpaka ukamilike na
wengine kukubali kuupokea mradi huo.
Walisema kuwa,
hawakubalimakabidhiano ya mradi huo mpaka kasoro zilizopo kama
vile kurekebisha maeneo ya mtaro unaosambaza maji sehemu ambazo
zimebomoka na hivyo kusababisha maji kupotelea ardhini zilekebishwe , kujenga
mtaro wa maji hadi eneo lililolengwa katika msitu wa Rwamulazi ardhi
ya kijiji ambapo ndipo unapatikana mto mwisa ambao utasaidia upatikanaji wa
maji mwaka mzima.
Amani Ndabatunga ni mkazi wa kijiji
cha Bujuruga kata ya Bugene kabla ya mradi kukabidhiwa kwa wananchi alihoji
kuhusiana na eneo ambalo lilikuwa limelengwa ambalo ni ardhi ya kijiji
na kuwa halmashauri ina mpango gani wa kufikisha mtaro wa maji katika
eneo lililolengwa tofauti na sasa kwani
mtaro unaishia kwenye maeneo ya watu binafsi ambapo
alijibiwa kuwa muarobaini ni fedha iliyoombwa kutoka Japani.” Kwanza mradi huu
haukuwa hitaji letu na hatukuwahi kushirikishwa katika mapato na matumizi”.
Alisema Ndabatunga.
Naye diwani wa Kata ya Bugene
Alistides Mulilo aliwasawishi wananchi katika kijiji hicho ili wakubali
kukabidhiwa mradi wao ili waanze kufaidi matunda ya mradi huo kwa kupanda
mbogamboga kama vile nyanya, kabeji, nyanyachungu, vitunguu Karoti na
mbogamboga nyingine kwa kukubaliana na wenye
maeneo ambapo mtaro wa kusambaza maji unapita wakati wakisubili eneo
lililolengwa la kilimo cha umwagiliaji wa mpunga miundo mbinu yake
ikamilike.
Deodatus Kinawilo mkuu wa wilaya ya
Karagwe alisema kuchelewa kukamika kwa mradi huo kulisababishwa na madiwani
wenyewe kwani kiasi cha fedha kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya mradi huo
kiasi cha shilingi milioni 600 walizitumia kulipana posho na matumizi mengine
kinyume cha utaratibu “ Nilisha mueleza mkurugenzi mtendaji kurudisha fedha
hizo haraka ili mradi uendelee na ukamilike.
Ikumbukwe kuwa, mradi wa kilimo cha
umwagiliaji wa mpunga Mwisa kijiji cha Bujuruga uliibuliwa na
wananchi wa kijiji hicho mwaka 2007 na kuanza rasmi mwaka 2011 ambapo ilibidi
ukamilike mwaka 2012.
Post a Comment