Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MWALIMU MKUU AVULIWA WADHIFA WAKE KWA KOSA LA KUCHELEWA MKUTANO WA MKUU WA WILAYA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butinzya, amevuliwa wadhifa huo kwa madai ya kuchelewa kuhudhuria kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Wila...

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butinzya, amevuliwa wadhifa huo kwa madai ya kuchelewa kuhudhuria kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Amani Mwenegoha.

Utekelezaji wa kumvua madaraka mwalimu huyo, Mathias Mazuri, ulifanywa na Ofisa Elimu Shule za Msingi wa wilaya hiyo, Shadrack Kabanga.

Mwalimu Mazuri alichelewa kikao kilichoitishwa na Mwenegoha Februari 6, kikiwa na lengo la kudhibiti fedha za ruzuku ya Serikali na kwamba adhabu hiyo ni fundisho kwa watumishi wengine.

Akitangaza kumvua wadhifa huo mbele ya walimu wakuu wenzake, Kabanga alisema Shule ya Butinzya ipo karibu na eneo la mkutano na wezake waliotoka mbali walifika saa 3:00 asubuhi yeye saa 6:00 mchana.

“Sikubali, huu ni muda wa kubadilika siyo kuleana, nakuvua wadhifa kuanzia sasa siyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butinzya,” alisema.

Mwalimu Mazuri alijitetea kuwa kuchelewa kwake kulitokana na pikipiki yake kuharibika njiani, utetezi huo ulitupiliwa mbali na ofisa elimu.

Mkuu wa wilaya hiyo, Mwenegoha aliwataka walimu kutumia vizuri fedha za ruzuku na kwamba, wasichangishe wazazi kutokana na uhaba wa posho za madaraka.

Mwenegoha alipiga marufuku kuwadai wanafunzi fedha za masomo ya ziada.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. mhhhhh uwezi jua alikua akifanya nini wenyewe wanafanya kitu bila thinking yoyote

    ReplyDelete

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top