Home
»
News
» JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
____________________________________________
UTANGULIZI
Ndugu
wanahabari, Wizara imepokea taarifa kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya
Shinyanga imevamia ofisi za shirika la Jhpiego mkoani humo na kukamata baadhi
ya watumishi wake kwa madai ya shirika hilo kugawa mafuta maalumu yanayodhaniwa
kutumiwa kuhamasisha ngono za jinsia moja. Baada ya taarifa hiyo wizara
inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
Si
kweli kwamba shirika la Jhpiego limekuwa likihamasisha ngono baina ya wapenzi
wa jinsia moja. Shirika hilo kupitia mradi wa "Sauti" linasaidia
serikali katika jitihada za kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa
makundi yaliyopo kwenye hatari kubwa ya maambukizi. Moja ya makundi
yanayolengwa ni wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao. Shirika limekua
likitoa elimu ya mabadiliko ya tabia kwa wanaume hao huku likiwapatia mafuta
hayo kama sehemu ya kuwasaidia kupunguza hatari ya maambukizi.
Mafuta
hayo yaliingizwa nchini kwa kufuata taratibu za kisheria kwa ufadhili wa Mfuko
Maalumu wa Rais wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI
(PEPFAR).
Ndugu
wanahabari, kama mtakumbuka hivi karibuni Wizara kupitia kwa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ilisitisha ugawaji
wa mafuta hayo maalumu (vilainishi) miongoni mwa makundi hayo maalumu.
Kufuatia
agizo hilo, Wizara iliagiza Shirika hilo kukusanya mafuta hayo na kuyarudisha katika
ofisi za PEPFAR zilizopo Ubalozi wa Marekani ili yapelekwe katika nchi nyingine
zinazofadhiliwa na PEPFAR ambazo matumizi ya mafuta hayo hayazuiwa.
Ndugu
wanahabari, Shirika hilo lilitekeleza agizo la wizara la kukusanya mafuta hayo
na kuyaweka katika ofisi zao za kanda, tayari kuyasafirisha kuja jijini Dar es
Salaam, ambapo umeandaliwa utaratibu maalumu wa kuyapeleka katika nchi nyingine
bila kuyaharibu.
Mnamo
tarehe 27 mwezi July, mwaka 2016 Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Shinyanga
ilivamia Ofisi za Shirika hilo na kuchukua mafuta hayo bila kuelewa utaratibu
uliotolewa na Wizara wa kukusanya mafuta hayo na kuyarudisha katika ofisi za
PEPFAR.
Zoezi
hilo la kamati ya Ulinzi na Usalama halikushirikisha wizara ya Afya wala wadau
wa sekta ya Afya wilayani humo, ambao wanaelewa vizuri utaratibu uliowekwa na
wizara kukusanya mafuta hayo na kuyarudisha mahali husika bila kuyaharibu.
Ndugu
wanahabari, tayari Wizara imeshamuandikia barua Katibu Tawala wa Mkoa wa
Shinyanga kutaka mafuta hayo yaliyochukuliwa kurudishwa katika ofisi za mradi
wa Sauti zilizopo mtaa wa Mwasele, kata ya Kambarage mkoani Shinyanga ili zoezi
la kuyakusanya na kuyarudisha Dar es Salaam liweze kuendelea.
Mwisho,
Wizara inapenda kuwajulisha kuwa shirika la Jhpiego ni miongoni mwa wadau wakuu
wa Serikali ambao wamekuwa wakisaidia huduma mbalimbali za Afya nchini ikiwemo
kusaidia ujenzi wa vituo vya afya, kupambana na maambukizi ya virusi vya
UKIMWI, kuboresha Afya ya mama na mtoto na Uzazi wa Mpango kwa zaidi ya miaka
kumi sasa. Hivyo serikali imeridhia shirika hilo kuendelea kutoa huduma
mbalimbali za afya bila kutumia mafuta hayo.
Imetolewa
na:
Michael
O. John
Kaimu
Katibu Mkuu,
Wiza
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Related Posts
- KAGERA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUENDELEA KUJIIMARISHA KUWALINDA RAIA NA MALI ZAO25 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya ...Read more »
- MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA ZA KARAGWE NA NGARA PIA HITIMISHO WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa ku...Read more »
- MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI KAGERA NA KUANZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YABILIONI 1216 Apr 20180
Na: Sylvester Rapahel Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na...Read more »
- TIMU YA WATAALAM WA UJENZI KUTOKA NCHINI CHINA YAKAGUA ENEO LA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA ILI KUANZA UJENZI MARA MOJA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Serikali ya Watu wa China yatuma timu ya Wataalam wa Usanif...Read more »
- MKOA WA KAGERA WAVUKA LENGO KATIKA UNDIKISHAJI WA WANAFUNZI AWALI NA DARASA LA KWANZA MWAKA 201816 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika madarasa...Read more »
- MKUU WA MKOA KAGERA AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUFIKISHWA OFISINI KWAKE AKIWA NA PINGU MIKONONI BAADA YA KUITIA SERIKALI HASARA08 Mar 20180
Na Sylvester Raphael Mkuu wa Mkoa wa Kagera aagiza Mkandarasi wa Kampun...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.