Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: SIMANZI KWA TASNIA YA HABARI TANZANIA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Simanzi,siku moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumfunga miaka kumi na mitano askari ya aliyemuua Daudi Mwangosi,tasnia ya ha...


Simanzi,siku moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumfunga miaka kumi na mitano askari ya aliyemuua Daudi Mwangosi,tasnia ya habari yapata pigo,mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya Mwangosi,SHUJAA JOSEPH SENGA,amefariki dunia usiku huu.

Senga amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo.

Bila Joseph Senga,shujaa aliyehatarisha maisha yake,akasimama bila woga,akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi wenye silaha,huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi,milio ya risasi ikisikika,na kuzitunza,zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi,leo hii asingekuwa Senga,nadhani  kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu dhidi ya aliyemuua Mwangosi.Nakulilia Senga..

Senga,Senga,Senga,Senga,umekwenda,Mungu aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho  amekuchukua,Senga umekwenda wadogo zako katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.

Senga,Senga,kamsalimie Daudi Mwangosi,mwabie aliyemuua nae kahukumiwa jela miaka 15,kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu.


Nenda Senga,picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top