Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habati kutoka Afrika Kusini ikiwemo mtandao wa KickOff, Ngoma amesaini mkataba huo baada ya kufuzu vipimo vya afya katika klabu hio na anatarajiwa kujiunga nao mata baada ya mkataba wake na Yanga kuisha mwishoni mwa mwezi huu.
Alisajiliwa na Yanga kama mchezaji huru mwaka 2015 akitokea Platnum Fc ya nchini kwao Zimbabwe.
Msimu uliopita licha ya kusumbuliwa na majeraha, Ngoma aliifungia Yanga mabao 8 katika mechi 18 za Ligi alizocheza, alicheza kwa jumla ya dakika 1394.
Y
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.