Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WORLD VISION KAGERA WAONESHA MFANO WAMUUNGA MKONO MKUU WA MKOA WA KAGERA KATIKA KAMPEINI YAKE YA KUPANDA MITI YA MATUNDA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Na: Sylvester Raphael Shirika lisilo kuwa la Serikali World Vision Tanzania Kanda ya Kagera limemuunga Mkono Mkuu wa Mkoa wa...


Na: Sylvester Raphael



Shirika lisilo kuwa la Serikali World Vision Tanzania Kanda ya Kagera limemuunga Mkono Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Kampeini yake ya kupanda miti ya matunda katika Mkoa wa Kagera ili kuondoa tatizo la udaumavu, utapiamulo na  kwashakoo kwa wananchi wa Kagera hasa watoto.


Shirika la World Vision Kanda ya Kagera limeto kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Miche 200 ya miti ya matunda aina mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 2,000,000/= na Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliikabidhi miche hiyo kwa Taasisi za Shule katika Manispaa ya Bukoba ili ikapandwe kwenye mazingira ya Taasisi hizo.




Akikabidhi miche ya matunda Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Kagera  Bibi Juliana Charles alisema wameamua kummunga mkono Mkuu wa Mkoa katika juhudi zake za kuhakikisha miti ya matunda inapandwa na matunda yanapatikana kwa wingi ili kuhamasisha wananchi kula matunda na kupunguza udumavu, utapiamulo na kwashakoo hasa kwa watoto.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akipokea miche hiyo alilishukuru shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Kagera kwa kutoa misaada ya mara kwa mara na kushirikiana na Serikali  katika shughuli mbalimbali za kuondoa umasikini na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera.


“World Vision wamekuwa wa msaada kwa Mkoa wetu wa Kagera, nakumbuka  wakati wa Tetemeko Shirika hili lilikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha hali za wananchi zinarejeshwa haraka sana, pia kampeini hii niliizindua tarehe 26 Januari, 2018 lakini unaweza kuona sasa tayari wameitikia wito na kuniunga mkono nawashukuru sana,” Alishukuru Mhe. Kijuu



Aidha, Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu alitoa wito kwa Taasisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali kumuunga mkono katika kampeini ya kupanda miti ya matunda  ambapo alisema kuwa miche ya miti ya matunda ina gharama kubwa kidogo kwani kila mche mmoja  unauzwa kwa gharama ya shilingi 10,000/= jambo ambalo mwananchi wa kawaida yawezekana asimudu gharama ya kununua lakini Taasisi zikijitolea wananchi wanaweza kugawiwa miche hiyo bure na wakaipanda.





Tayari Mkuu wa Mkoa ameagiza kila mwananchi kupanda miche mitano ya matunda katika eneo lake pia na Taasisi zote zihakikishe zinapanda miche ya matunda katika maeneo yao. World Vision Tanzania Kanda ya Kagera wamekabidhi miche ya matunda  200 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Februari 26, 2018.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top