WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali ya awamu ya tano inafanya kila
juhudi kuhakikisha uchumi wake unamilikiwa na wananchi, nia ikiwa ni
kuifanya nchi kuwa na uchumi wa kati.
Majaliwa
aliyasema hayo jana, wakati akizindua mpango wa uwezeshaji wananchi
kiuchumi, ambao pamoja na mambo mengine utatoka na mapendekezo ya nini
cha kufanya kufikia malengo yake.
Kwa
mujibu wa waziri mkuu, ili kufikia malengo ya mkakati huo, wadau wote
hawana budi kuunganisha nguvu pamoja kuanzia ngazi ya juu hadi chini.
“Taarifa
zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki
uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha
kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo
zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.
Aidha
alizitaja mojawapo ya nyenzo muhimu katika kufanikisha suala hilo ni
pamoja na uhakika wa masoko, riba nafuu kwa wajasiriamali, pamoja na
ushirikishwaji wa viongozi wote.
“Napenda
mkimaliza mkutano wenu mnipatie mapendekezo ya kile mlichokubaliana
hapa, kwani nimekuwa na utaratibu kila nikifanya ziara zangu mikoani
lazima nizungumze na wananchi na huwa nawaeleza haya masuala ya mipango
ya serikali katika kuwawezesha,” alisema waziri mkuu.
Awali
akimkaribisha waziri mkuu, Waziri wa Nchi Ofi si ya Waziri Mkuu Sera,
Uratibu, Bunge, Uwezeshaji, Ulemavu Vijana na Wazee, Jenister Mhagama,
alisema kuwa kuwawezesha wananchi ni hatua muhimu katika maendeleo ya
taifa.
Katika
kufanikisha azma hiyo, Waziri Jenister alisema tayari serikali
imefanikiwa kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji, ambapo vijana na
wananchi kwa ujumla watapewa kipaumbele zaidi.
“Mikoa
20 tayari imeshatenga maeneo na sasa wanaweka miundombinu ambayo nia
yake ni kuwasaidia wananchi kuweza kumiliki uchumi wao,” alisema.
Hatahivyo
mojawapo ya changamoto inayokabili utekelezaji wa sera ya uwezeshaji
wananchi kiuchumi ni ukosefu wa ajira na umasikini, ambavyo vinalikabili
kundi hili muhimu.
Imeelezwa
kuwa maeneo ambayo yanatajwa kama sehemu muhimu zenye kuwezesha
kupatikana kwa matokeo ya haraka ni sekta ya utalii, ujenzi,
usafirishaji, kilimo, madini, misitu na viwanda.
Post a Comment