Wauguzi kote
nchini wanaungana
na wauguzi wenzao
duniani kuadhimisha siku
ya wauguzi ambayo ni
kumbukumbu ya Muuguzi wa
Kwanza Frolensi Mitingale ambaye ni
muasisi wa siku
hiyo kwa kuelezea
umma changamoto na mazingira
magumu ya wauguzi
ambayo aliyapitia kwa
kuwasha mishumaa kuhudumia
watu.
Akiongea na Redio Fadeco afisa muuguzi wa hospitali teule ya Nyakahanga wilaya ya Karagwe
Laingitoni Kishebuka amesema kuwa chimbuko la siku ya wauguzi duniani ni
kumbukumbu ya muuguzi wa kwanza Frolensi
Mitingale aliyehasisi huduma hii ya kiuguzi.
Kishebuka amesema licha ya kuwa siku hii huadhimishwa Mei12 lakini wauguzi wa wilaya ya Karagwe wao
wataadhimisha siku hiyo Ijumaa ya Mei13 mwaka huu katika uwanja wa mpira Changarawe ulipo
mjini Kayanga ambapo wauguzi kutoka hospitali ya Nyakahanga wataungana na
wauguzi wa kituo cha afya Kayanga kusherekea siku hiyo.
Ameongeza kuwa maandamano yataanzia katika hospitali ya
Nyakahanga hadi kituo cha afya Kayanga ambapo watawatembelea wagonjwa
waliolazwa kituoni hapo kwa ajili ya kuwasalimia na kuwapa zawadi siku hiyo.
Hata hivyo baadhi wauguzi wameshauriwa kutanguliza
uzalendo kwanza wanapokuwa wanawahudumia wagonjwa licha ya changamoto mbalimbali
zinazowakabili.
Siku ya wauguzi ambayo itaazimishwa kesho itaongozwa na
kauli mbiu inayosema kuwa wauguzi nguvu ya mabadiliko katika kuboresha huduma
za afya kwa jamii.
Post a Comment