Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WALIMU ILI KUONGEZA UFAULU
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wazazi   na   walezi   wametakiwa   kutoa   ushirikiano   kwa   walimu kwa   kufuatilia   mienendo   kwa   watoto   wao   ili   kuweza  ...

Wazazi  na  walezi  wametakiwa  kutoa  ushirikiano  kwa  walimu kwa  kufuatilia  mienendo  kwa  watoto  wao  ili  kuweza  kuongeza  ufaulu  katika  masomo  yao  kuliko  kuwaachia  walimu  pekee  yao  kwani  wanafunzi  inabidi  kulelewa  na  panfde  zote  mbili.

Wito  huo  umetolewa  leo   na  mwalimu  wa  Taalumu   Katarina  Ernest   wa    shule  ya  msingi  Lukole  iliyopo  kata  ya  Ihanda  wilayani  Karagwe  wakati  akitoa  hali  ya  taaluma  ya  shule  hiyo  kwenye  mkutano  wa  wazazi  uliofanyika  shuleni  hapo.

Amesema  kutokana  na  kukua  kwa  maendeleo  haswa  kuletwa  umeme  na  baadhi  ya  wananchi  kununua  televisheni  kumechangia  utoro  mwingi  maana  wanafunzi  hushinda  kwenye  vinabanda  wakiangalia michezo  mbalimbali.
Ernest  amesema  wao  wanatimiza  wajibu  wao  kwa  mujibu  wa  taratibu  za  kazi  lakini  wameongeza  jitihada  zaidi  na  kujitolea  muda  wa  ziada  bila  malipo  lakini  hawawezi  kufanikiwa  bila  ushirikiano  wa  wazazi  kwa  walimu.

Kwa  upande  wake  mwalimu  mkuu  wa  shule  ya  Lukole   Jonester  Rwiza  amesema  kuwa  kutokana  na  utoro  wa  mara  kwa  mara  wamechukua  hatua  kwa  kuongea  na  wazazi  na  walezi  wenye  watoto  hao  wamewafikisha  kwenye  baraza  la  kata  ya  Ihanda.

Aidha  katibu  wa  kamati  ya  uji  shuleni  hapo   Venanti  Katabazi  ametoa  taarifa  ya  hali  ya  wanafunzi  kupata  uji  shuleni  hapo  amesema  kuwa  walikuwa  wamelengwa  wanafunzi 509  waliochangia  ni  281 ,waliomalizia  michango  ni 101 ,wanaodaiwa 180 na  wasiochangia  chochote  ni 228  ambao   ni  changamoto  kwa  shule  hiyo.

Diwani  wa  kata  hiyo  Januari  Joackimu  amewataka  wazazi  na  walezi  kujenga  utamaduni  wa  kupenda  kujadili  namna  ya  kuongeza  kasi  ya  maendeleo  kwenye  shule,kijiji  na  kata  kwa  ujumla  ili  kuondoa  hali  iliyopo  ya  malumbano  yasiyokuwa  na  tija  yoyote  ile.

Aidha  amewataka  kuhakikisha  wanachangia   maendeleo  ikiwemo  kukamilisha   utengenezaji  wa  madawati 250    ambayo  yanahitajika  katani  humo, lakini  akagusia  kuwepo  kwa  changamoto  ya  matundu  ya  vyoo  kujaa  na  Zahanati  ya  kijiji  hicho.

Hata  hivyo  ametumia  fursa  hiyo  kuwataka  watu  wote  wenye  maeneo  kwenye kata  hiyo  yeliyo  vipara  kuhakikisha  wanapanda  miti  ili kuhifadhi  mazingira  na  kuwataka  pia  kutovuna  kahawa  mbichi  vinginevyo  watachukuliwa  hatua kali  za  kisheria.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top